Na Magreth Mbinga
Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mh Nape Mosses Nnauye amesema hakuna amani,furaha na maendeleo katika jamii kama kuwepo kwa Uhuru wa vyombo vya habari.
Kauli hiyo ameitoa katika ufunguzi wa kongamano la maendeleo ya sekta ya habari ambalo limekusanya wadau mbalimbali wakiwemo wakufunzi wa habari, wanafunzi wa taaluma ya habari kutoka katika vyuo mbalimbali,Afisa habari wa Serikali na Binafsi .
“Nimuhimu sana tukahakikisha Uhuru wa habari unalindwa kama msingi wa maendeleo wa amani na furaha katika jamii yetu “amesema Mh Nape.

Pia Nape amewapongeza kwa uteuzi wa mada za kongamano hilo kama maendeleo ya vyombo vya habari ,uongozi na uzalendo sheria mbalimbali katika sekta ya habari ,mafanikio na changamoto katika sekta ya habari ,Mawasiliano ya kimkakati ,uandishi wa habari wa kujenga ,mjadala wa mchango ambao unangazia sekta ya habari katika maendeleo ya sekta zingine kama tehama,afya ,kilimo,miundombinu,elimu ,demokrasia na kadhalika.

Aidha Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Godwin Gondwe ambae amemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh Amos Makala amesema Mkuu wa Mkoa anatambua umuhimu wa habari na Wakazi wengi wa Dar es Salaam wanafatilia sana habari hasa maudhui ya mtandao.
“Hakuna mipango ya maendeleo inayopangwa bila mpango mkakati kuandaliwa kwa kongamano hili Mh Waziri umefanya jambo kubwa sana sababu hata matajiri wakubwa Duniani wamewekeza katika teknolojia ya Mawasiliano“amesema Gondwe.
Sanjari na hayo Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile amesema vyombo vya habari vimefanya kazi kubwa ya kuunganisha Taifa baada ya uhuru kupitia lugha ya kiswahili .
“Hapa sote tunazungumza kiswahili hata umoja wa Taifa letu umetokana na kiswahili na kazi hii imefanywa na vyombo vya habari lakini pia kumekuwa na sheria mbalimbali za vyombo vya habari ambazo ninasaidia kukuza lugha hiyo“amesema Balile.








