Home Kitaifa NMB YAZINDUA PROGRAM YA MUDA KATI (MULTICURRENCYMEDIUM TEAM NOTE MNT)

NMB YAZINDUA PROGRAM YA MUDA KATI (MULTICURRENCYMEDIUM TEAM NOTE MNT)

Na Magrethy Katengu

BANKI ya NMB leo Septemba 25, imezindua rasmi Programu ya Muda wa Kati (Multicurrency Medium Term Note – MTN) yenye thamani ya Sh. Trilioni 1, pamoja na kufungua Dirisha la Uwekezaji wa Toleo la Kwanza la Hati Fungani ya Jamii (NMB Jamii Bond).

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi huo jijini Dar es Salaam, Msajili wa Hazina, Nehemia Mchechu amesema Serikali inajivunia bunifu za viwango vya NMB, huku Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Nicodemus Mkama, akiitaja Hati Fungani hiyo kuwa ya kwanza kwa ukubwa Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Awali, Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna, amesema benki hiyo inaanza kuiuza rasmi Jamii Bond kote nchini kuanzia Septemba 25 hadi Oktoba 27 mwaka huu, na baada ya hapo itapatikana katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), kwa wanunuzi watakaoikosa katika kipindi hicho.

“NMB Jamii Bond ni ya kipindi cha miaka mitatu, hadi Novemba 2026, ambako wawekezaji wake watapata riba ya asilimia 9.5 kwa mwaka na italipwa kwa vipindi vinne kwa mwaka. Kiasi cha chini ni Sh. 500,000 na mnunuzi atapaswa kujaza fomu matawini na kwa Mawakala wa DSE waliopewa kibali na CMSA.

“Wanunuzi wa Hati Fungani hii ni watu wote, binafsi, mashirika, makampuni, lengo ni kukusanya Sh. Bilioni 75, lakini CMSA imeturuhusu kufanya ongezeko (green shoe option) la Sh. Bilioni 25, kwa hiyo tunaweza kwenda hadi Sh. Bilioni 100.

“Tumeruhusiwa na CMSA kuuza Hati Fungani hii kwa shilingi za Kitanzania, lakini pia kwa Dola za Kimarekani, ambako tumepewa idhini ya mauzo ya Dola Milioni 10 na ongezeko la Dola milioni 5, hivyo kufanya mauzo ya Dola kuwa yanayoweza kufikia Milioni 15.

“Fedha zitakazopatikana zitatumika kutoa mikopo inayolenga matokeo chanya na endelevu katika jamii, ikiwemo kwa ajili ya miradi ya nishati mbadala, miradi ya kuzuia na udhibiti wa uchafuzi mazingira, usimamizi wa maji safi na maji taka na miradi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

“Pia itakuwa ni kwa ajili ya mikopo ya kuwawezesha wanawake na usawa wa kijinsia, ya nyumba nafuu, usalama wa chakula, huduma za afya, elimu, vijana,” alibainisha Bi. Zaipuna huku akizishukuru taasisi zote zilizoshirikiana nao, zikiwemo Benki Kuu ya Tanzania (BoT), CMSA, DSE, ABSA Tanzania ambayo ni Mshauri Mwenza.

Naye Mchechu, aliwashukuru washirika wa mchakato huo, hususani wasimamizi BoT, CMSA na DSE kwa walichofanya kufanikisha jambo kubwa na la kihistoria kutokea katika Sekta ya Fedha nchini, ambacho ni kitu cha kujivunia na kujipongeza.

“Kazi nzuri inayofanywa na NMB, inaipa Ofisi ya Msajili heshima tukiwa ndio wasimamizi wa Sekta ya Fedha. Sisi kama Serikali tunafurahia sana uwekezaji wetu ulioko NMB, tunajivunia na ndio ‘model’ ambayo tutaitumia na kuiingiza katika Taasisi na Mashirika yetu, kwa sababu tumeiona faida yake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!