Na Shomari Binda-Musoma
MADAKTARI bingwa wa magonjwa mbalimbali ya binadamu wanatarajiwa kutoa huduma za kibingwa kwa wananchi wa manispas ya Musoma na vitongoji vyake.
Huduma za madaktari hao kuwaona wananchi zitatolewa kwa kwenye hospital ya CF iliyopo mjini Musoma ikiwa ni kumbukumbu ya miaka 2 ya kifo cha aliyekuwa mkurugenzi na muasisi ws hospital hiyo Dk.Emanuel Chacha.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mjini hapa,meneja wa hospital hiyo bw.Noel Chacha ,amesema huduma za madaktari hao zitatolewa siku ya jumamosi mei 27 kwenye hospital hiyo.
Amesema Dk.Chacha alikuwa na malengo makubwa katika kutoa huduma za afya kwa wananchi tangu kuanzishwa kwa hospital novemba 2018 hivyo katika kumuenzi wameamua kuwafikia wananchi.
Meneja huyo amesema magonjwa yatakayofanyi wa uchunguzi kwa siku hiyo ni magonjwa ya mfumo wa moyo,.magonjwa ya damu,mfumo wa mkojo,watoto,mazoezi ya viungo, magonjwa ya ngozi,mfumo wa koo na pua,magonjwa ya ndani pamoja na magonjwa ya wanawake.
Amesema madaktari hao watatoa huduma kwa wagonhws wenye bima za afya na hata wasiokuwa na bima.
“Kwa wasiokuwa na bima watapata nafasi ya kuonana na madaktari Bure lakini watachangia gharama za dawa na vipimo vya maabara“
“Madaktari bingwa watakuwepo hapa CF hospital kuja kutoa huduma kwa wananchi ikiwa ni kumbukumbu ya miaka 2 ya Dk.Chacha ambaye alikuwa na dhamira ya kutoa huduma za afya”
“Hii ni fursa ambayo wananchi wa Musoma na vitongoji vyake wanapaswa kuitumia kuja kufanya uchunguzi wa afya”,amesema








