Na Boniface Gideon, TANGA
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba Jana amekabidhi msaada wa vyakula kwa makundi maalumu yenye Mahitaji Maalumu wakiwemo Wazee wasiojiweza na Watoto yatima.
Vituo vilivyonufaika na msaada huo ni pamoja na Kituo Cha Wazee wasiojiweza Duga, Kituo Cha Watoto yatima Cha Good Will mwahako na Kituo Cha kulea Watoto yatima Cha Ansar Makorora huku makundi yote yakinufaika na Mchele,Mafuta,mbuzi,maharage na Vinywaji , Msaada huo ni kwaajili ya kusherekea sikukuu ya Eid Elifitr .
Akikabidhi msaada huo ,Rc Kindamba Alisema Ofisi yake imeona sio jambo zuri kusherekea sikukuu ya Eid bila kuwakumbuka Watu Wenye Mahitaji Maalumu,
“Tumeona sio jambo zuri kusherekea sikukuu kwa furaha Wakati Kuna wenzetu wanahitaji ,tumeamua tuungane kwa pamoja kuhakikisha tunasherekea sikukuu kwa furaha”Alisisitiza Kindamba
Katika hatua nyengine, mkuu huyo wa Mkoa aliahidi kuzifanyia kazi changamoto zilizopo kwenye vituo hivyo hususani Kituo Cha lelea Wazee wasiojiweza Duga ambacho miundombinu yake imechakaa ,
“Sitaki kuwa msemaji Sana naomba tukazifanyie kazi changamoto hizi ,nimeambiwa miundombinu ya Umeme ni mibovu ,Majengo pia machakavu na mengine mengi tutayafanyia kazi” alibainisha RC Kindamba
Mwisho








