Home Kitaifa DIWANI WA KATA YA PASIANSI ASHIRIKI UJENZI WA ZAHANATI

DIWANI WA KATA YA PASIANSI ASHIRIKI UJENZI WA ZAHANATI

Diwani wa kata ya Pasiansi wilaya ya Ilemela Rosemary Mayunga ameshiriki zoezi la kuchimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati inayotarajiwa kujengwa katika mtaa wa Bwiru Press katani humo kwa nguvu za wananchi lengo likiwa ni kupunguza umbali mrefu wa kufuata huduma za afya kwa kina mama na watoto.

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Bwiru Press, wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza Edina Ntahondi ameipongeza Serikali ya awamu ya sita kwa kutoa fedha za ujenzi wa Zahanati katika mtaa wake ambapo amesema, wananchi watapata huduma za afya kwa ukaribu bila kuwa na usumbufu wowote mara itakapokamilika.

Mwenyekiti wa CCM kata ya Pasiansi Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza Kawawa Magumba amesema, kujengwa kwa Zahanati ya Bwiru Press itasaidia kusogeza huduma kwa taasisi za shule za Bwiru boys, Bwiru girls, Kitangiri sekondari, shule ya msingi Bwiru, kituo cha watu wenye ualibino pamoja na chuo cha Mipango na wananchi waliokuwa wanakwenda km 7 kuzifikia huduma za afya katani humo.

Wananchi wa mtaa wa Bwiru Press wamepongeza jitihada zilizofanywa na diwani wa kata ya Pasiansi Wilaya ya Ilemela MkoanI Mwanza Rosemary Mayunga kwa kuhamasisha ujenzi wa Zahanati katika mtaa huo ambayo itasaidia kuondoa hadha ya upatikanaji wa huduma ya afya katika eneo hilo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!