Home Kitaifa MAAFISA BIASHARA WATAKIWA KUCHOCHEA UCHUMI WA VIWANDA

MAAFISA BIASHARA WATAKIWA KUCHOCHEA UCHUMI WA VIWANDA

NAIBU Waziri wa Viwanda na Biashara, Dennis Londo,akizungumza wakati wa Mkutano wa Kati ya Wizara na Wakuu wa Sehemu na Idara za Viwanda,Biashara na Uwekezaji katika Sekretariet za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kinachofanyika kuanzia leo Agosti 17 hadi 18 jijini Dodoma.

NAIBU Waziri wa Viwanda na Biashara, Dennis Londo,akizungumza wakati wa Mkutano wa Kati ya Wizara na Wakuu wa Sehemu na Idara za Viwanda,Biashara na Uwekezaji katika Sekretariet za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kinachofanyika kuanzia leo Agosti 17 hadi 18 jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Balozi Waziri Salum,akizungumza wakati wa Mkutano wa Kati ya Wizara ya Viwanda na Biashara na Wakuu wa Sehemu na Idara za Viwanda,Biashara na Uwekezaji katika Sekretariet za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kinachofanyika kuanzia leo Agosti 17 hadi 18 jijini Dodoma.

 Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Godfrey Nyaisa,akizungumza wakati wa Mkutano wa Kati ya Wizara ya Viwanda na Biashara na Wakuu wa Sehemu na Idara za Viwanda,Biashara na Uwekezaji katika Sekretariet za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kinachofanyika kuanzia leo Agosti 17 hadi 18 jijini Dodoma.

SEHEMU ya washiriki wakimsikiliza Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Dennis Londo (hayupo pichani) ,akizungumza wakati wa Mkutano wa Kati ya Wizara na Wakuu wa Sehemu na Idara za Viwanda,Biashara na Uwekezaji katika Sekretariet za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kinachofanyika kuanzia leo Agosti 17 hadi 18 jijini Dodoma.

SEHEMU ya washiriki wakimsikiliza Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Dennis Londo (hayupo pichani) ,akizungumza wakati wa Mkutano wa Kati ya Wizara na Wakuu wa Sehemu na Idara za Viwanda,Biashara na Uwekezaji katika Sekretariet za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kinachofanyika kuanzia leo Agosti 17 hadi 18 jijini Dodoma.

NAIBU Waziri wa Viwanda na Biashara, Dennis Londo,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kugungua Mkutano wa Kati ya Wizara na Wakuu wa Sehemu na Idara za Viwanda,Biashara na Uwekezaji katika Sekretariet za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kinachofanyika kuanzia leo Agosti 17 hadi 18 jijini Dodoma.

NAIBU Waziri wa Viwanda na Biashara, Dennis Londo,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kugungua Mkutano wa Kati ya Wizara na Wakuu wa Sehemu na Idara za Viwanda,Biashara na Uwekezaji katika Sekretariet za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kinachofanyika kuanzia leo Agosti 17 hadi 18 jijini Dodoma.

NAIBU Waziri wa Viwanda na Biashara, Dennis Londo,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kugungua Mkutano wa Kati ya Wizara na Wakuu wa Sehemu na Idara za Viwanda,Biashara na Uwekezaji katika Sekretariet za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kinachofanyika kuanzia leo Agosti 17 hadi 18 jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA

NAIBU Waziri wa Viwanda na Biashara, Dennis Londo, amewataka Maafisa Biashara nchini kutumia nafasi zao kikamilifu kuibua fursa za uwekezaji, kuongeza thamani ya mazao na kuboresha mazingira ya biashara katika halmashauri, hatua inayolenga kuchochea maendeleo ya kiuchumi na utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Londo ametoa kauli hiyo leo Agosti 17,2026 jijini Dodoma  wakati wa Kikao cha Tatu cha Wizara ya Viwanda na Biashara na Maafisa Biashara nchini, kilicholenga kuimarisha utekelezaji wa majukumu yao katika kukuza biashara, viwanda na uwekezaji.

Amesema Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 inalenga kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha uchumi wa viwanda katika Afrika Mashariki na Kati, ikiwamo kufikia uchumi wa dola trilioni moja na kuongeza kipato cha Mtanzania hadi dola 7,000. Amesema kufikia malengo hayo kunahitaji uchumi imara, jumuishi na shindani unaotegemea sekta binafsi, sayansi na teknolojia, uwekezaji, utafiti pamoja na nguvu kazi yenye ujuzi.

“Maafisa Biashara wana jukumu la kuhakikisha halmashauri zinakuwa vituo vya uzalishaji, uwekezaji na biashara kwa kutambua fursa zilizopo, kuwaunganisha wazalishaji na masoko na kuhakikisha mazao yanaongezwa thamani. “amesema Mhe.Londo

Hata hivyo ametolea mfano wa mahindi, amesema wakulima wanapaswa kusaidiwa kuondokana na kuuza mazao ghafi na badala yake kuzalisha bidhaa kama unga wenye chapa na kuufikisha kwenye masoko, hatua itakayoongeza kipato na kuchangia kupunguza umaskini.

Aidha, amesema utekelezaji wa Dira 2050 unahitaji vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kushirikishwa kikamilifu katika uzalishaji, uwekezaji na biashara kupitia fursa za mikopo na uwezeshaji. Amesema katika mwaka wa fedha 2025/2026, viwanda vikubwa vipya 25 vilijengwa katika sekta mbalimbali na kutoa ajira 39,000, zikiwamo ajira 7,600 za moja kwa moja na 31,000 zisizo za moja kwa moja.

Katika kuimarisha mazingira ya uwekezaji, Londo amezitaka mikoa kuhuisha kanzidata za viwanda, biashara, masoko, leseni, wawekezaji na maeneo yaliyotengwa kwa shughuli za kiuchumi, huku kila halmashauri ikiandaa wasifu wa fursa za uwekezaji unaoonyesha upatikanaji wa malighafi, miundombinu, masoko na maeneo ya uwekezaji. Pia amewataka Maafisa Biashara kuhakikisha Mabaraza ya Biashara yanafanya kazi kikamilifu na hoja za sekta binafsi zinapatiwa ufumbuzi kwa wakati.

Katika hatua nyingine, Londo amewataka Maafisa Biashara kuharakisha urasimishaji wa biashara zisizo rasmi kwa kutoa elimu kuhusu usajili wa biashara, leseni, TIN, viwango, vipimo na taarifa za umiliki.

Amesema urasimishaji utawawezesha wafanyabiashara kupata huduma za uwezeshaji, mitaji na masoko, huku akieleza kuwa halmashauri zimetengewa asilimia tano ya mapato ya ndani, yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 72 kwa mwaka wa fedha 2026/2027, kwa ajili ya kuwekeza katika miundombinu ya masoko, maeneo ya biashara na ujasiriamali.

Amesisitiza fedha hizo zitumike kwa ufanisi kwa kushirikisha sekta za ardhi, maji, nishati na barabara ili kuongeza tija kwa wafanyabiashara na kuvutia wawekezaji. Aidha, amewataka Maafisa Biashara kutumia nafasi zao kuboresha huduma na kuifanya Tanzania kuwa na mazingira bora zaidi ya biashara na uwekezaji, hatua ambayo ni muhimu katika kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Balozi Waziri Salum, amewataka Maafisa Biashara kuongeza udhibiti wa bidhaa feki na viwanda visivyo rasmi katika maeneo yao, akieleza kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kulinda afya na usalama wa wananchi, watumiaji pamoja na wazalishaji wanaofuata sheria.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Godfrey Nyaisa, amesema Maafisa Biashara ni kiungo muhimu kati ya Serikali na wafanyabiashara katika kuhakikisha sera, sheria na kanuni za biashara zinatekelezwa na kuleta mabadiliko chanya katika mazingira ya biashara na uwekezaji nchini.

Amesema kuelekea utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, BRELA imeendelea kuboresha mifumo na sheria zinazosimamia usajili na utoaji wa leseni kwa lengo la kupunguza muda na gharama za kuanzisha na kuendesha biashara. Amesema kupitia BRELA Online System (ORS), huduma za wakala zimeunganishwa katika mfumo mmoja, huku mfumo huo ukiwezesha pia utoaji na usimamizi wa leseni za biashara kundi A na B.

Amesema mfumo huo unatoa fursa kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa kutoa na kusimamia leseni za kundi B bila kuathiri mapato yao, kwani malipo yanayofanywa na mfanyabiashara yanaingia moja kwa moja katika akaunti ya halmashauri husika.

Aidha, ORS imeunganishwa na mifumo ya taasisi nyingine za Serikali ikiwamo NIDA na TRA, hatua inayowezesha taarifa muhimu kupatikana moja kwa moja bila mfanyabiashara kuwasilisha nyaraka ambazo tayari zipo kwenye mifumo hiyo.

Nyaisa,amesema kuwa  maboresho hayo yameongeza uwazi na ufanisi, kupunguza urudufu wa taarifa, muda na gharama za kupata huduma, pamoja na kupunguza mianya ya uzembe katika utoaji wa huduma.

“BRELA itaendelea kushirikiana na Wizara ya Viwanda na Biashara, Ofisi ya Waziri Mkuu–TAMISEMI, sekretarieti za mikoa na halmashauri katika kuwajengea uwezo Maafisa Biashara.”amesema Nyaisa

Amesema katika mwaka wa fedha 2026/2027, BRELA imepanga kutoa mafunzo kwa Maafisa Biashara wote nchini kupitia kanda nne, yatakayolenga matumizi ya mifumo, utoaji na usimamizi wa leseni pamoja na utekelezaji wa sheria.

Pia amesema BRELA itaendelea kuboresha miunganiko ya mifumo ya kidijitali na kushirikiana na vyama vya Maafisa Biashara katika kutatua changamoto zao, huku akisisitiza kuwa maafisa hao ni mawakala muhimu wa uwekezaji nchini na wanapaswa kutambua kuwa jukumu lao ni kuwezesha biashara, si kuikwamisha, ili kujenga mazingira rafiki kwa wafanyabiashara na wawekezaji.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!