Home Kitaifa VITONGOJI VYOTE MTWARA KUFIKISHIWA UMEME – WAZIRI NDEJEMBI

VITONGOJI VYOTE MTWARA KUFIKISHIWA UMEME – WAZIRI NDEJEMBI

📌Zaidi ya Bilioni 203 zatumika kufikisha Umeme kwenye Vijiji mkoani Mtwara

Serikali kupitia Wizara ya Nishati imeahidi kutafuta fedha kuhakikisha Vitongoji vyote mkoani Mtwara vinafikishiwa umeme.

Ahadi hiyo, imetolewa leo na Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi wakati wa hafla ya kuwasha umeme katika Kitongoji cha Maendeleo iliyofanyika katika Shule ya Sekondari ya Mtiniko iliyopo katika Kijiji cha Mtiniko, Wilaya ya Mtwara mkoani Mtwara.

“Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan alitoa fedha kwa ajili ya kuhakikisha Vijiji pamoja na Vitongoji ambavyo bado havijapata umeme vipate umeme. Na leo tumekuja kuuwasha umeme huo.

Mkoa wa Mtwara pekee umeletewa zaidi ya Shilingi Bilioni 203 kwa ajili ya kukamilisha upelekaji wa umeme kwenye vijiji na vitongoji vyake. Nanyamba hapa kuna vijiji 87 na vijiji vyote vimepata umeme. Lakini pia, hapa kuna vitongoji 324, na vitongoji 306 tayari vina umeme. Vitongoji 8 tayari Wakandarasi wanaendelea na kazi. Tunakwenda kutafuta fedha za vitongoji 10 vilivyosalia,” amesema Waziri Ndejembi.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba amesema kuwa Wizara ya Nishati itaendelea kuhakikisha wananchi wanapata umeme ulio bora.

Awalia akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya kupeleka umemem kwenye vijiji pamoja na vitongoji kwa Mkoa wa Mtwara, Mkurugenzi wa Umeme Vijijini kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Jones Olotu amesema kuwa Mkoa wa Mtwara una jumla ya vijiji 785 ambavyo vyote tayari vina umeme.

Kwa upande wa vitongoji, Mhandisi Olotu amesema kuwa, Mkoa wa Mtwara una jumla ya vitongoji 3421 ambapo Serikali kupitia REA imefanikiwa kufikisha umeme katika vitongoji 2839 huku jitihada mbalimbali za kuhakikisha vitongoji vyote vinapatiwa umeme.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!