Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza linawashilikia watu 9 kwa tuhuma za makosa mbalimbali ikiwemo wizi wa vifaa vya ujenzi katika mradi wa reli ya kisasa SGR pamoja na ujenzi wa daraja la Magufuli maarufu Kigongo – Busisi.Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza Wilbroad Mutafungwa amesema, watu hao wamekamatwa kufuatia operesheni iliyoanza tarehe 11.January mwaka huu katika maeneo ya vijiji vya Isunga, Nkalalo, Bukwimba, Malya, na Usagara Wilayani Kwimba na Misungwi.

Aidha Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa watatu wakiwa na Pikipiki mali ya Omary Shabani dereva bodaboda iliyoibiwa kisesa wilayani Magu Mkoani Mwanza yenye namba za usajili MC 450 DLM yenye rangi nyeusi baada ya kuvamiwa na kuporwa katika kijiji cha Mwamanyiri Kamanda Mutafungwa amesema

Jeshi hilo pia linaendelea ma msako mkali wa kutafuta watuhumiwa wa wizi wa watoto wawili wachanga katika maeneo mawili tofauti, walioripotiwa kuibiwa.









