

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeaihidi kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania Bara na Zanzibar kwa kutumia bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania(TEMDO) ili kuongeza matumizi ya teknolojia za ndani,
kukuza uchumi na kupunguza gharama za kununua bidhaa nje ya nchi.
Hayo yalisemwa Oktoba 18, 2025 na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk, Said Seif Mzee akiwa ameambatana na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar, Dkt. Mohamed Dhamir Kombo, wakati walipotembelea TEMDO Jijini Arusha.

Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda yaSerikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk, Said Seif Mzee , ameisitiza TEMDO kuzalisha mitambo ya kuongeza thamani mazao pamoja na mitambo ya kutengeneza vifungashio ili kuwawezesha Wajasiliamali wa Tanzania kuhimili ushindani katika soko na kutimiza Malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar, Dkt. Mohamed Dhamir Kombo ameisisitiza TEMDO kuendelea kuzalisha bidhaa bora , za uhakikika na kuziuza kwa bei nafuu ili wakulima wengi waweze kujikwamia kiuchumi kwa kuuza bidhaa zilizoongezwa thamani.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Abdallah, amesema ushirikiano huo utaongeza ufanisi wa maendeleo ya viwanda na kuongeza tija katika matumizi ya teknolojia za ndani na kuchochea uchumi wa Taifa.
Naye, Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TEMDO Profesa Lazaro Busagala amebainish kuwa Temdo inazalisha bidhaa zaidi ya 16 ikiwemo vifaa tiba vya hospitali Kama majokofu ya kuhifadhia maiti, vichomea taka hatarishi, vitanda vya aina mbalimbali vinavyohitaji kufika soko la Zanzibar ili kuongeza patio la Taifa, kukuza uchumi na kupunguza uagizaji wa bidhaa hizo kutoka nje ya nchi.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa TEMDO Profesa Fredick Kahimba amasema Taasisi hiyo inaendelea kubuni teknolojia mbalimbali ikiwemo teknolojia ya mazao ya baharini katika sekta ya uvuvi ikiwemo mashine za kukausha dagaa, jokofu (cold room) la kuhifadhia samaki nyama na mbogamboga.