Home Kitaifa TEKNOLOJIA ITALINDA MILA NA TAMADUNI – DKT. SAMIA

TEKNOLOJIA ITALINDA MILA NA TAMADUNI – DKT. SAMIA

Mgombea wa Nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa miaka mitano ijayo itakuwa ni miaka ya ujenzi wa Tanzania ya teknolojia na yenye kuenzi na kuzingatia maadili ya jamii, akiomba ridhaa ili kutekeleza kikamilifu dhamira hiyo ya maendeleo nchini.

Akizungumza na wananchi Mtwara Mjini kwenye muendelezo wa Kampeni zake za kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 katika Uwanja wa Saba saba, Dkt. Samia ameahidi kwamba miaka mitano ijayo ataongeza matumizi ya teknolojia za kisasa ikiwemo ujumuishaji wa akili unde katika kilimo na sekta nyingine ili kuimarisha ufanisi na tija katika uzalishaji na utoaji wa huduma ikiwemo kwenye kilimo, pamoja na kufundisha teknolojia ili watoto wapate elimu hiyo kuendana na mahitaji.

Tunataka kuunganisha teknolojia, mila, tamaduni na desturi zetu kwa kufundisha teknolojia ambayo haitafuta, kuharibu ama kupotosha vijana wetu wakakiuka mila na desturi zetu. Tunataka kwa kadri itakavyowezekana, teknolojia ikalinde mila, tamaduni na desturi zetu na tuzirithishe kwa kikazi kijacho.” Amesema Dkt. Samia.

Katika hatua za awali za kufanikisha suala hilo Dkt. Samia ameitaja sekta ya kilimo kama kipaumbele zaidi akisema tayari kwenye serikali ya awamu ya sita alizindua maabara kubwa Mjini Dodoma na nyingine Sokoine Morogoro, akisisitiza pia uanzishaji wa vituo vya zana za kisasa za kilimo kwaajili ya wakulima pamoja na uendeshaji wa minada kwa njia ya mtandao, vipimo pamoja na uimarishaji wa mawasiliano na mifumo ya ufuatiliaji wa hali ya hewa katika kufanikisha kilimo cha kisasa chenye kutumia teknolojia kukuza uzalishaji na ubora wa mazao ya Kilimo nchini.

Tangu kuzinduliwa ka Kampeni za Chama Cha Mapinduzi Jijini Dar Es Salaam, Dkt. Samia kando ya Mgombea mwenza wake tayari amefanya mikutano ya kampeni kwenye Mikoa takribani 15 ya Kanda ya Kati, Kusini, Kusini Magharibi pamoja na Mikoa miwili ya Kanda ya Ziwa sambamba na Visiwani Zanzibar, akitarajiwa sasa kuingia kwenye Mikoa ya Pwani na baadae Kanda ya Kaskazini ikiwemo Mkoa wa Arusha anapotarajiwa mwanzoni mwa mwezi wa Kumi, mwezi wa mwisho kuelekea uchaguzi Mkuu wa Jumatano ya Oktoba 29, 2025.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!