Viongozi wa dini wameaswa kuwa daraja kati ya viongozi wa Serikali na wananchi ili kuhakikisha changamoto zao zinatatuliwa pamoja na kulinda amani ya nchi katika kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa pamoja na uchaguzi mkuu.
Hayo yamesemwa na Mbunge wa Jimbo la Ulanga mkoani Morogoro wakati akishiriki ibada ya pasaka katika kanisa la Roma Kwiro wilayani Ulanga ambapo amesema ni wakati sasa wa kulinda amani ya nchi
Pia Mbunge huyo amewataka wazazi kuzingatia maadili wakati wa makuzi ya watoto wao.