Home Kitaifa SERIKALI KUCHUKUA HATUA ZA KINIDHAMU KWA WAAJIRI WOTE WASIOZINGATIA SHERIA

SERIKALI KUCHUKUA HATUA ZA KINIDHAMU KWA WAAJIRI WOTE WASIOZINGATIA SHERIA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete, akizungumza na  watumishi wa Tume ya Utumishi wa Umma na Mamlaka za Maji Tanzania  wakati akifungua mafunzo ya namna bora ya Utekelezaji wa Sheria ya Utumishi wa Umma na Matumizi ya Mfumo wa kielektroni wa kushughulikia Rufaa na uwasilishwaji wa taarifa za masuala ya kiutumishi kilichofanyika katika ukumbi wa NSSF Mkoani Morogoro, tarehe 9 February, 2026. 

Na Antonia Mbwambo – Morogoro

Serikali imetoa onyo kali kwa Waajiri, Mamlaka za Ajira na Mamlaka za Nidhamu katika Utumishi wa Umma zitakazoshindwa kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria, ikisisitiza kuwa haitasita kuchukua hatua za kinidhamu dhidi yao.

Onyo hilo limetolewa leo tarehe 9 Februari, 2026 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete, wakati wa ufunguzi wa kikao kazi kati ya Tume ya Utumishi wa Umma na Mamlaka za Maji nchini. Kikao hicho kililenga kujadili utekelezaji wa Sheria ya Utumishi wa Umma Sura ya 298, matumizi ya mfumo wa kielektroniki wa kushughulikia rufaa na malalamiko pamoja na uwasilishaji wa taarifa za kiutumishi kwa Tume.

Mhe. Kikwete amesema kuwa Waajiri, Mamlaka za Ajira na Mamlaka za Nidhamu wanapaswa kuwasilisha vielelezo vya rufaa na malalamiko kwa Tume ya Utumishi wa Umma kwa wakati, kama sheria inavyoelekeza.

“Ninatoa rai kwa Waajiri wote, Mamlaka za Ajira na Mamlaka za Nidhamu kuwasilisha vielelezo vya rufaa na malalamiko kwa Tume ya Utumishi wa Umma kwa wakati. Vinginevyo, Serikali haitasita kuchukua hatua za kinidhamu dhidi yao,” amesema Mhe. Kikwete

Amefafanua kuwa vielelezo hivyo vinaweza kuwasilishwa kupitia Mfumo wa Kielektroniki wa Kushughulikia Rufaa na Malalamiko katika Utumishi wa Umma na Uwasilishaji wa Taarifa za Kiutumishi (PSCMIS).

Mhe. Kikwete ameeleza kuwa baadhi ya Waajiri na Mamlaka husika wamekuwa wakishindwa kutekeleza wajibu wao ipasavyo, hususan pale Tume inapowaelekeza kuwasilisha vielelezo vya rufaa na malalamiko, hali inayosababisha watumishi wa umma kucheleweshewa haki zao na Serikali kupata hasara.

Hata hivyo ameongeza kuwa pale muda wa kuwasilisha vielelezo unapopitwa, Tume hulazimika kuamua rufaa kwa kutumia vielelezo vya upande mmoja kwa kuzingatia sheria, jambo ambalo si sahihi kwani halitendi haki kwa warufani, walalamikaji pamoja na Serikali iliyotoa dhamana kwa Mamlaka hizo kusimamia Utumishi wa Umma.

Mhe. Kikwete, amesema uwepo wa mifumo ya TEHAMA unaimarisha utawala bora kwa kuwawezesha warufani kufuatilia kwa urahisi hatua iliyofikiwa katika rufaa na malalamiko yao.

Aidha, amesisitiza kuwa Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imepewa dhamana ya kuhakikisha dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kujenga Utumishi wa Umma wenye uadilifu, uwajibikaji na utoaji wa huduma bora kwa wananchi inatekelezwa kikamilifu kupitia Tume ya Utumishi wa Umma.

Katika hatua nyingine, Mhe. Kikwete amewashukuru Waandishi wa Habari kwa kuendelea kuhabarisha umma kuhusu jitihada za Serikali katika kuimarisha haki za Watumishi wa Umma na kuendeleza misingi ya Utawala Bora nchini.

Viongozi wa Tume ya Utumishi wa Umma wakimsubiri Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete kuwasili katika katika kikao kazi cha mafunzo ya Tume ya Utumishi wa Umma  kwa Mamlaka za Maji Tanzania, tarehe 9 Februari, 2026

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete,akisalimiana na Viongozi wa Tume ya Utumishi wa Umma baada ya kuwasili katika Ofisi za NSSF Mkoani Morogoro katika ufunguzi wa mafunzo ya Utekelezaji wa Sheria ya Utumishi wa Umma na Matumizi ya Mfumo wa kielektroni wa kushughulikia Rufaa na uwasilishwaji wa taarifa za masuala ya kiutumishi kwa Tume hiyo kwa Washiriki kutoka Mamlaka za Maji Tanzania, tarehe 9 Februari, 2026.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete, akizungumza na  watumishi wa Tume ya Utumishi wa Umma na Mamlaka za Maji Tanzania  wakati akifungua mafunzo ya namna bora ya Utekelezaji wa Sheria ya Utumishi wa Umma na Matumizi ya Mfumo wa kielektroni wa kushughulikia Rufaa na uwasilishwaji wa taarifa za masuala ya kiutumishi kilichofanyika katika ukumbi wa NSSF Mkoani Morogoro, tarehe 9 February, 2026. 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete (kushoto) akiteta jambo na Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma Jaji Mstaafu Mhe. Hamisa Kalombola, wakati wa kikao kazi cha mafunzo ya Tume ya Utumishi wa Umma  kwa Mamlaka za Maji Tanzania cha Utekelezaji wa Sheria ya Utumishi wa Umma na Matumizi ya Mfumo wa kielektroni wa kushughulikia Rufaa na uwasilishwaji wa taarifa za masuala ya kiutumishi leo tarehe 9 Februari, 2026.

Washiriki wa mafunzo ya Tume ya Utumishi wa Umma kwa Mamlaka za Maji Tanzania cha Utekelezaji wa Sheria ya Utumishi wa Umma na Matumizi ya Mfumo wa kielektroniki wa kushughulikia Rufaa na uwasilishwaji wa taarifa za masuala ya kiutumishi wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) wakati Waziri huyo alipokuwa akizungumza nao leo Mkoani Morogoro.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Tume ya Utumishi wa Umma baada ya Waziri huyo kufungua kikao kazi cha mafunzo ya Tume ya Utumishi wa Umma kwa Mamlaka za Maji Tanzania cha Utekelezaji wa Sheria ya Utumishi wa Umma na Matumizi ya Mfumo wa kielektroniki wa kushughulikia Rufaa na uwasilishwaji wa taarifa za masuala ya kiutumishi leo tarehe 9 Februari, 2026

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!