Home Kitaifa RITA YATAKIWA KUTOA VYETI VYA KUZALIWA NDANI YA SAA 48

RITA YATAKIWA KUTOA VYETI VYA KUZALIWA NDANI YA SAA 48

Na Halima Issa,

Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) imetakiwa kutekeleza mpango wa utoaji wa vyeti vya kuzaliwa ndani ya saa 48 za kazi, hatua inayolenga kuwawezesha wananchi kupata huduma nyingine kwa wakati, hususan zile zinazohitaji cheti cha kuzaliwa.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Juma Homera, wakati wa uzinduzi wa mpango huo jijini Dar es Salaam, akisisitiza kuwa utekelezaji wake unapaswa kusimamiwa kwa weledi ili kutoa huduma bora kwa wananchi.

Ameeleza kuwa utekelezaji wa mpango huo ni sehemu ya maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, aliyesisitiza vyeti vya kuzaliwa vitolewe ndani ya saa 48 za kazi.

Waziri huyo ameongeza kuwa mchakato wa kupata cheti cha kuzaliwa utakuwa rahisi kwa waombaji watakaokuwa na viambatanisho muhimu, ikiwemo barua ya Serikali ya Mtaa, taarifa kutoka hospitalini pamoja na vielelezo kutoka taasisi za dini kama misikiti na makanisa.

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!