Mkuu wa mkoa wa Songwe Mhe. Daniel Chongolo amefanya ziara katika Halmashauri ya Mji Tunduma ambapo ametembelea Hospitali ya Mji Tunduma na kujionea namna ya utoaji huduma ya madaktari bigwa wabobezi wa Mhe. Rais Dr. Samia Suluhu Hassan katika hospitali hiyo.

Mhe. Chongolo amefanya ziara hiyo Jumanne Mei 14, 2024 ikiwa ni siku moja baada ya Mkoa wa Songwe kupokea madaktari bingwa ambao wametawanywa kutoa huduma za kibingwa na bobezi katika Halmashauri tano za mkoa huu.
Mhe. Chongolo aliambatana na watendaji wa serikali wa Mkoa wa Songwe akiwepo Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe Bi Happiness Seneda pamoja na katibu Tawala Wilaya Bw.Frank Nkindwa








