Na Boniface Gideon, TANGA
Serikali imesema Bandari ya Tanga haipo kwenye Mpango wa kuwekwa wawekezaji wa ndani au nje hivyo Wananchi wa Mkoa wa Tanga wasiwe na wasiwasi.
Kauli ya Serikali inakutokana na sakata la Bandari ya Dar es Salaam kuonekana kuwa gumzo hasa kwenye mitandao ya kijamii huku wakazi wa Mkoa wa Tanga Wengi wao walikuwa wakihoji Nini hatma ya Bandari ya Tanga Baada ya kufanyiwa maboresho makubwa ikiwamo uchimbaji wa kina Cha Bahari, Ujenzi wa magati pamoja na ununuzi wa mitambo ya kisasa ya upakua na upakiaji wa mizigo Bandarini hapo.
Pia Waziri Mbarawa aliwatahadharisha Watumishi wa Umma kuzingatia Maadili ya kazi zao na kujiepusha na vitendo visivyofaa ikiwamo uvujishaji wa Siri za Serikali nakwamba wote waliohusika na Uvujishaji wa Siri za Serikali watatafutwa na kuchukulia hatua huku akionekana kushangaa mkataba huo kusambazwa Sasa hivi Wakati ni wamuda mrefu.
Waziri Mbarawa aliyasema hayo Leo Wakati akizungumza na Watumishi wa Menejimenti ya Wizara ya Ujenzi na Menejimenti za Taasisi za Wizara hiyo kwenye kikao kazi Cha Cha Siku tatu kilichofanyika mkoani Tanga.
Waziri Mbarawa Alisema Bandari ya Tanga haimo kwenye Mpango wa kutafutiwa mwekezaji kutokana na kujimudu kiutendaji ,
“Kwa Bandari ya Tanga haipo kwenye Mpango wa kutafutiwa mwekezaji kwakuwa Haina changamoto,tulichokifanya nikuifanyia maboresho makubwa na tutaleta mitambo mingine ya kisasa zaidi ili iwe na ufanisi mkubwa zaidi ya hapa kwahiyo Wananchi wasiwe na wasiwasi juu ya Hilo” aisisitiza Prof. Mbarawa
Alisema kuwa Bandari ya Dar es Salaam imetafutiwa mwekezaji kwa magati mawili Kati ya 12 ili kuongeza Teknolojia kubwa zaidi ya utendaji kazi Bandarini hapo,
“Kampuni tuliyoingia nayo mkataba ndio kampuni kubwa Duniani kwenye na imewekeza zaidi ya Nchi 30 kwahiyo Jamii isipotoshwe juu ya Hilo” Alisisitiza Mbarawa
Aidha akizungumzia sakata la nyaraka za Siri za mkataba wa Bandari ya Dar es Salaam na kampuni ya DP zilizozagaa mitandaoni ,
“Watumishi jiepusheni na vitendo vya kuvujisha Siri za Serikali, ukivujisha ni lazima ukamatwe kwakuwa Teknolojia ni kubwa sana,mpo hapa kwaajili ya kueleza changamoto zenu fungukeni na kueleza changamoto zenu msiogope ili tukitoka hapa kila mmoja wetu akatekereze majukumu yake vizuri” Alisema Mbarawa
Kufuatia kauli ya Serikali juu ya Bandari ya Tanga kutokubinafsishwa kwa mwekezaji Baadhi ya Wakazi wa Tanga waliishukuru Serikali kwakutomweka mwekezaji,
“Sisi kama Wananchi hususani wa maeneo haya ya Bandari tulikuwa na wasiwasi juu ya Bandari yetu na vibarua vyetu hapa Bandarini Mana tunayaona kwenye mitandao tu juu ya Bandari ya Dar es Salaam” Alisema Hassan Jamal mkazi wa Tanga Mjini
Mwisho










