Na. Mwandishi wetu Jeshi la Polisi.
Jeshi la Polisi mkoani Arusha lipo katika mkakati wa kuanzisha klabu za kupinga ukatili na unyanyanyasajii wa kijinsia katika shule zote mkoani humo.
Hayo yamesemwa leo februari 24, 2023 na Mkuu wa Polisi Jamii mkoani Arusha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP Sammy Magige wakati akizungumza na Wakaguzi wa kata pamoja na wakuu wa madawati ya jinsia jijini humo katika kikao kazi kilichofanyika ukumbi wa trafiki Arusha.

SSP Magige amebainisha kuwa kupitia klabu zitakazoanzishwa, wanafunzi watapata fursa ya kufundishwa mambo mbalimbali kuhusiana ukatili wa kijinsia ambapo watatumia elimu hiyo kwenda kuwafundisha wanafunzi wengine namna bora ya kuzuia na kuripoti vitendo vya ukatili.
Sambamba na hilo pia amesema kupitia Askari kata ambao wamekua wakitoa elimu katika maeneo mbalimbali, imepelekea wananchi kuanza kuyaibua matukio ya ukatili kwa wingi.
Aidha amewataka wakaguzi hao kuendelea kutoa elimu katika maeneo yote ili wananchi waendelee kufichua matukio ya uhalifu na wahalifu ili mkoa huo uendelee kuwa salama.
Toka Dawati la Habari Mkoa wa Arusha.








