Home Kitaifa ORYX GASI WAUNGA MKONO JITIHADA ZA SERIKALI KUTHIBITI UKATAJI MITI KWA KUGAWA...

ORYX GASI WAUNGA MKONO JITIHADA ZA SERIKALI KUTHIBITI UKATAJI MITI KWA KUGAWA MITUNGI 3600 ILI KUPUNGUZA MATUMIZI YA KUNI NA MKAA PWANI

Na Scolastica Msewa

Mitungi ya majiko ya gasi ya Kampuni ya Oryx 3600 imegaiwa kwa Wananchi wa mkoa wa Pwani ikiwa ni mpango wa Kampuni hiyo kuunga mkono jitihada za serikali za kuthibiti ukataji miti na utunzaji wa mazingira na kupunguza matumizi ya kuni na mkaa.

Akitoa mada kwa Wafanyabishara wauza gasi za Oryx wa Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani Afisa masoko wa Kampuni ya Oryx Evarest Kisaka amesema mitungi hiyo imetolewa kwa ushirikiano na Wakala wa Umeme vijijini REA ambao walitoa mitungi 1800 na Kampuni hiyo pia imetoa mitungi 1800.

Amesema mitungi hiyo imekabidhiwa kwa Wabunge wa majimbo ya mkoa wa Pwani ambayo watagawa kwa Wananchi wake.

Kisaka amesema udhibiti wa ukataji miti na utunzaji wa mazingira husaidia kuthibiti mabadiliko ya tabia nchi ambayo hupelekea uhaba wa mvua na kuleta athari kwa jamii.

“Tunajua wote kwamba mvua zisiponyesha njaa inakuwa kali na njaa ikishakuwa kali ni mzigo kwa taifa hivyo Serikali inapambana kutoa elimu na kutoa mitungi ya majiko ya kuanzia kwa Wananchi wasio tumia gasi lengo tu Watanzania tuachane na matumizi ya nishati isiyo rafiki” amesema Kisaka.

“Tunaona ni jinsi gani serikali inahimiza Wananchi waachane na nishati ambayo sio rafiki kwa matumizi ya binadamu ambapo ukiachana na Serikali kupitia REA na Kampuni hiyo ya Oryx lakini pia Kuna shirika la kimataifa la UN nao pia hushiriki kutoa mitungi hiyo ya majiko kwa Wananchi nchini”

Naye Afisa Masoko wa Kampuni ya ECO Africa Abdullatif Jafar Abeid amewataadhalisha Watumishi wa majiko ya gasi kuzingatia vifaa vyenye ubora ili kujilinda na matukio ya moto majumbani.

Amesema mitungi wa gasi uweke mita zaidi ya mbili kutoka kwenye jiko ili kujilinda na kujihakikisha usalama wao na Mali zao kwa kutumia vifaa vyenye ubora na madhubuti.

Kamanda wa jeshi la Zimamoto Wilaya ya Mkuranga Francisco Chunji amewataka wenye ya kufanya biashara ya uuzaji wa mitungi ya gasi kufika kwenye Ofisi za jeshi hilo ilikupata elimu ya namna sahihi ya kutoa huduma kwa Wananchi huku wakijilinda na majanga ya milipuko ya moto wao na wateja wanaowahudumia.

Amesema kuna sababu mbalimbali za mitungi ya gasi kulipuka hivyo wauzaji ni muhimu wakafundishwa vizuri ili wakawafundishe na wateja wao ambao ndio watumiaji wa gasi majumbani wakati wanawauzia mitungi hiyo madukani kwao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!