Home Kitaifa MATHAYO AELEZEA UMUHIMU WA ELIMU KWA WAHITIMU KAMNYONGE SEKONDARI, AWAAHIDI “PRINTER NA...

MATHAYO AELEZEA UMUHIMU WA ELIMU KWA WAHITIMU KAMNYONGE SEKONDARI, AWAAHIDI “PRINTER NA PHOTOCOPY”

Na Shomari Binda-Musoma

MBUNGE wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo amewahimiza wahitimu wa kidato cha nne shule ya sekondari Kamnyonge kuipa umuhimu elimu kwa kuwa ndio muongozo wa dunia ya leo.

Kauli hiyo imetolewa na diwani wa Kata ya Kamnyonge David Cosmas kwa niaba yake kwenye mahafali ya 12 ya shule hiyo.

Amesema kwenye dunia ya leo elimu inayo nafasi kubwa hivyo wahitimu wa kidato cha 4 wa shule hiyo wasione walipofikia ndio mwisho.

Mathayo amesema ajira na nafasi nzuri serikalini na hata mashirika binafsi yanazingatia vigezo vya elimu ili kuweza kupata nafasi.

Amesema wapo watakaoendelea na kidato cha 5 na watakaoenda vyuoni hivyo lazima wakazingatie ili kufikia ndoto zao.

” Kwenye mahafali haya alipaswa awepo mbunge lakini ameniagiza kuja kumuwakilisha kwa kuwa yupo kwenye vikao.

” Kubwa amesema niwasisitize kuzingatia na kuishika elimu kwa kuwa kwenye dunia ya leo inayo nafasi kubwa katika kuajiliwa na hata kujiajili”,amesema.

Aidha muwakilishi huyo wa mbunge amesema moja ya maombi kwenye risala yao mbunge amewaahidi kuwanunulia mashine ya printer na photocopy ili kuweza kudurufu mitihani yao wakiwa shuleni.

Aidha amesema kwa kuwa mbunge ameahidi vifaa hivyo yeye kama diwani atatoa computer kwaajili ya matumizi ya shule.

Mkuu wa shule hiyo Yese Itono Makulu amesema wanayo imani wahitimu wa mwaka huu kufanya vizuri kwa kuwa walimu wamewaandaa.

Amesema wanamshukuru mbunge na diwani kwa ahadi zao kwa kuwa zinakwenda kupunguza changamoto shuleni hapo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!