Home Kitaifa MAJI YAENDELEA KUPATIKANA KIGAMBONI, CHANG’OMBE, KARIAKOO NA MJINI

MAJI YAENDELEA KUPATIKANA KIGAMBONI, CHANG’OMBE, KARIAKOO NA MJINI

Na Secilia Edwin

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imetoa taarifa kuhusu kuendelea kwa upatikanaji wa huduma ya majisafi katika baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar es Salaam, yakiwemo Kigamboni, Chang’ombe, Kariakoo pamoja na maeneo ya katikati ya jiji.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na mamlaka hiyo leo Desemba 16, 2025, DAWASA imeeleza kuwa tanki la majisafi lililopo Kigamboni limefunguliwa, hatua iliyowezesha wakazi wa Chang’ombe, Kariakoo, Kigamboni na maeneo ya mjini kupata huduma ya maji kwa siku ya leo.

Aidha, mamlaka hiyo imewahimiza wakazi wa maeneo yanayopata huduma ya maji kuhakikisha wanachota maji ya kutosha na kuyahifadhi ipasavyo kwa matumizi ya sasa na ya baadaye.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!