Na Theophilida Felician Kagera.
Ikiwa ni juhudi za kuendeleza kasi ya utekelezaji wa mpango wa malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto hapa nchini Mkoa Kagera kwa kushirikiana na wadau mbalimbali umeendelea kuchanja mbuga kwakuyafikia makundi tofauti tofauti katika kueneza dhana nzima ya utekelezaji wa mpango huo kwa jamii ambapo leo hii Tarehe 27 Septemba imewafikia Madiwani kutoka Manispaa ya Bukoba pamoja na Halmashauri ya Bukoba.

Ikitolewa elimu ya mpango huo kwa Madiwani hao kutoka kwa Afisa maendeleo ya jamii Mkoa Kagera Issa Mrina katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa Kagera Manispaa ya Bukoba amesema kuwa mpango huo unawajumuisha watu wote kwenye jamii hivyo nao kama madiwani ni sehemu ya kushiriki kusaidia utekelezaji wake katika maeneo yao.
Ameeleza kwamba mpango huo umejumuisha mambo kadha wakadha yenye kumlenga moja kwa moja mtoto hususani kwa upande wa malezi bora yenye muunganiko wa Elimu, Afya, lishe na usalama.
Katika maelezo yake amegusia suala la malezi kwa watoto lilivvyo changamoto kwa sasa katika jamii kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo wa watu kutokuwajibika ipasavyo hali ambayo imechochea baadhi ya watoto kuyapitia masaibu mengi yakiwemo ya kutendewa ukatili waina tofauti tofauti hususani ubakaji na ulawiti.
Ameendelea kufafanua kuwa malengo ya utekelezaji wa programu hiyo moja wapo ni kuboresha huduma muhumu kwa watoto pale ambapo huduma hizo hazikidhi mahitaji kwao.
“Utekelezaji wa hii programu ambayo niya mwaka 2021 mpaka 2025, 2026 itakuwa na sehumu ya matoke ya muda mfupi na matokeo ya muda mrefu ambapo katika hatua ya awali matokeo ya muda mfupi tunatarajia twende tukahamasishe jamii malezi yaliyo bora sisi ni Madiwani tunaishi kwenye jamii kule tunaona suala la maadili lilivyo huko nanijukumu letu kusema kama kuna mmomonyoko wa maadili tukaongee” ameeleza Afisa Maendeleo Issa Mrina.
Aidha katika matokeo ya muda mfupi pia amesema kuwa kunatakiwa kuonekana masuala mazima ya uratibu katika afua hizo za mtoto.
Katika matokeo ya muda mrefu ameyataja mengi yakiwemo ya kuona wazazi, walezi na jamii kwa ujumla wawe wamejengewa uwezo katika masuala mazima ya malezi bora.
“Tunasisitiza zaidi watoto walelewe kwenye familia zao isiwe mzigo wa mwalimu wakukulelea mtoto wako hawa watoto wanatakiwa walelewe katika ngazi ya familia” Amesisitiza Issa Mrina.
Amehitimisha akihimiza ushirikiano kwa kila mmoja kwa malengo ya kufanikisha adhima ya utekelezaji wa mpango huo.

Kwa upande wake Abemelek Richard akitokea Shirika la TADEPA ambao nimiongoni mwa wadau wanaoshirikiana na Serikali kwa ukaribu katika utekelezaji wa mpango huo akiwasilisha mada ya sayansi kupitia wasilisho la makuzi ya awali katika ukuwaji wa binadamu ameeleza kwanini mpango huo umewalenga watoto wakuanzia miaka 0- 8 kwani umri huo ni kipindi ambacho ni muhimu zaidi kwa ubongo wa mtoto kuwa katika hali imara ya uwezo wakuelewa vizuri kila jambo.
“Kwa hiyo katika makuzi ya awali ule umri wa awali nikipindi ambacho ujifunzaji unachukuwa nafasi kubwa, hivyo tunaishi miaka yetu 8 ambayo ikitumika vizuri kwa kipindi hicho mtoto atakuwa vyema hadi utu uzima wake” amesema Abemelek Richard.
Amevielezea vitu muhimu katika makuzi ya awali ya maisha ya binadamu nipamoja na lugha, tamaduni,hisia, kiimani, kiakili na kimwili.
Nao madiwani kwa umoja wao kupitia makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bukoba Privatus Anatory wameishukuru idara ya maendeleo ya jamii kwa kushirikiana na shirika la TADEPA kwa kuwapa elimu juu ya utekelezaji wa programu hiyo muhimu hivyo wameahidi kutoa ushirikiano wakuifikia jamii hadi ngazi ya chini kama ilivyo adhima ya Serikali na wadau huku wakikubaliana kulishirikisha shirika la TADEPA katika vikao vyao vya mabaraza ya madiwani ili liendelee kuwajenga kwa kuwapa elimu zaidi.








