Home Kitaifa KINANA AKUBALI KASI YA MAENDELEO MKOA WA MARA

KINANA AKUBALI KASI YA MAENDELEO MKOA WA MARA

Na. Shomari Binda-Musoma

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahaman Kinana ameonyeshwa kulidhishwa na kasi ya maendeleo inayoendelea mkoa wa Mara.

Kauli hiyo ameitoa kwenye uwanja wa shule ya msingi Mukendo alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara katika muendelezo wa ziara yake ya siku 10 hapa nchini.

Amesema amefika mkoa wa Mara na kupata taarifa nakujiona mabadiliko makubwa ya maendeleo yanayoendelea kwa kasi.

Kinana amesema miundombinu ya barabara, huduma za kijamii na hata uwanja wa ndege ni moja ya mabadiliko kwenye mkoa wa Mara.

Amesema kinachotakiwa kufanyika kwa sasa ni kushughulika na masuala ya kiuchumi ili wananchi waweze kunufaika

Makamu Mwenyekiti huyo amesema mkoa wa Mara ulikuwa na viwanda Vingi vikiwemo vya samaki,maziwa na nguo lakini leo vimekufa hivyo ni muhimu kuchukua hatua za kutosha kuvifingua.

Kinana amewataka viongozi wa CCM kutenga muda wa.kukutana na wananchi kuwasikiliza na kutatua kero zao.

Tangu nimeingia mkoa wa Mara nimeona mabadiliko makubwa ya kimaendeleo na niwapongeze viongozi wote kwa kusimamia shughuli za maendeleo”

“Nawaomba viongozi mtenge pia muda wa kwenda kuwasikiliza wananchi na kutatua matatizo yao na kero zao mziondoe kiungwana” amesema.

Akizungumzia suala la bandari,Kinana amesema hakuna bandari iliyouzwa bali ni baadhi ya wapotoshaji wanaopita na kupotosha.

Amesema Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan,namna anavyowapenda watanzania hawezi kusaini jambo ambalo halina manufaa na kudai elimu itaendelea kutolewa kwa wananchi ili kuwaondoa hofu.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vesastus Mathayo amemshukuru Makamu Mwenyekiti kwa ziara yake na kumuomba kumfikishia salamu na shukrani Rais Samia kwa namna anavyotoa fedha nyingi kwa shughuli za maendeleo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!