Home Kitaifa JESHI LA POLISI MKOANI MARA KUFANYA DORIA YA PAMOJA NA MAKAMPUNI YA...

JESHI LA POLISI MKOANI MARA KUFANYA DORIA YA PAMOJA NA MAKAMPUNI YA ULINZI

Na Shomari Binda-Musoma

JESHI la polisi mkoani Mara limesema lipo tayari kufanya doria ya pamoja na makampuni ya ulinzi ili kuwajengea uwezo wa uimalishaji ulinzi.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mara Kamishina Msaidizi wa Polisi(ACP) Salim Morcase ameyasema hayo wakati akizungumza na wamiliki wa makampuni ya ulinzi mkoani Mara.

Amewaomba wamiliki hao kuwaandaa askari wao kwa ajili ya kufanya doria ya pamoja kwa kushirikiana na jeshi la Polisi ikiwa ni pamoja na kupunguza uhalifu na vitendo vya kihalifu.

Akizungummza na wamiliki wa makampuni hayo yapatayo 24 katika ukumbi wa bwalo la polisi Mwisenge lililopo manispaa ya Musoma amesema ulinzi shirikishi ni jambo la msingi.

Morcase amewataka wamiliki hao wazingatie usalama wa walinzi wao kwa kuwapa silaha mbili kwa kila lindo, kuwasafirisha wakati wa kuwapeleka kwenye malindo na kuwaunga kwenye mifuko ya mafao.

“Kikao hiki ni muhimu katika kujengeana uwezo na niwashukuru wamiliki wa makampuni ya ulinzi kwa kuweza kufika na kuzungumza kwa pamoja”

“Pamoja na mengine yote askari wetu wanatakiwa kupata mafunzo ya mara kwa mara ili kuimalisha ulinzi kwenye malindo ili kudhibiti uhalifu”, amesema.

Aidha amesisitiza kuwa ili mlinzi aajiriwe ni lazima awe amepitia mafunzo ya mgambo au majeshi mengine hapa Tanzania na awe na uthibitisho wa hati ya tabia njema ili kuepuka kuajiri watu ambao ni wahalifu au ni raia wa kigeni.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa wamiliki wa makampuni hayo Charles Kingari Chama kwa niaba ya wamiliki hao amelishukuru jeshi la polisi kwa kuwa karibu nao na kuwapa elimu ambayo itawasaidia katika kuimarisha ulinzi na kuwa watoa taarifa wazuri wa taarifa za kihalifu na wahalifu pia kuzidisha ushirikiano ili kuhakikisha kuwa mkoa unaendelea kubaki salama.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!