Home Kitaifa MAABARA ZA SAYANSI ZAANZA KUJENGWA SHULE YA SEKONDARI NYANJA JIMBO LA MUSOMA...

MAABARA ZA SAYANSI ZAANZA KUJENGWA SHULE YA SEKONDARI NYANJA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI

Na Shomari Binda-Musoma

MAABARA 3 za masomo ya sayansi zimeanza kujengwa kwenye shule ya sekondari Nyanja iliyopo Kata ya Bwasi jimbo la Musoma vijijini.

Maabara zinazojengwa ni za kemia fizikia na bailojia ili kuwawezesha wanafunzi wa shule hiyo kujifunza masomo ya sayansi kwa vitendo.

Nyanja Sekondari ni ya Kata ya Bwasi yenye vijiji vitatu (3) vyenye jumla ya vitongoji ishirini na vitatu (23). Vijiji hivyo ni Bugunda, Bwasi na Bugunda.

Sekondari hii ilifunguliwa Mwaka 2006, na kwa sasa ina jumla ya wanafunzi 547, na walimu 12 wenye ajira, na 5 wa kujitolea.

Sekondari haina maabara hata moja na mwitikio wa wanafunzi kusoma masomo ya sayansi ni mdogo sana
Kwa mfano Kidato cha Nne (Form IV) chenye jumla ya wanafunzi 96, ni wanafunzi 13 tu wanaosoma somo la Fizikia.

Kwa kuona hilo mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini na Kamati ya Siasa ya Wilaya (CCM) waliendesha harambee ya kuanza ujenzi wa maabara za fizikia, kemia na baiolojia za sekondari hiyo.

Kwenye harambee hiyo fedha taslim shilingi 1,105,000 zilichangwa Saruji mifuko 141
Ikiwemo mifuko 100 ya mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Sospeter Muhongo.

Kamati ya Ujenzi ya watu wanne (4) imeundwa.mara baada ya haeambee hiyo ili iweze kufanikisha ujenzi wa maabara hizo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!