Home Kitaifa MBUNGE MATHAYO KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI KUIMARISHA USALAMA

MBUNGE MATHAYO KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI KUIMARISHA USALAMA

Na Shomari Binda-Musoma

MBUNGE wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Msthayo amesema ataendelea kushirikiana na jeshi la polisi mkoani Mara ili kuimalisha usalama.

Kauli hiyo ameitoa wakati akifunga mafunzo ya utayari kwa askari wakaguzi 32 katika kukabiliana na uhalifu na wahalifu pamoja na usalama wa raia na mali zao.

Amesema jeshi la polisi mkoa wa Mara limekuwa likifanya kazi nzuri katika kuimalisha usalama hivyo linahitaji ushirikiano.

Mathayo amesema kutokana na maelezo ya mafunzo waliyoyapata watakwenda kuongeza uwezo wa kufanya kazi ya kulitumikia taifa.

Amesema yeye kama mbunge ataendelea kushirikiana nao ili kuendelea kupata mafunzo ya utayari na kuwa imara.

“Niwapongeze askari ambao leo mmehitimu mafunzo na niwaahidi kuendelea kuwapa ushirikiano kwa wakati mwingine”

“Jimbo letu la Musoma mjini lipo salama na wananchi wameendelea kufanya shughuli zao za kiuchumi na niwashukuru sana jeshi la polisi”, amesema Mathayo.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Mara,Salim Morcase amesema mafunzo hayo ya miezi 2 yalikuwa na lengo la kuwaongezea askari wa kutimiza majukumu yao.

Kamanda huyo amemshukuru mbunge Mathayo kwa ushirikiano anao utoa kwa jeshi la polisi mkoani Mara katika kuimalisha ulinzi na usalama.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!