Home Kitaifa WAZAZI NA WALEZI WATAKIWA KUWAPA NAFASI YA KUPATA ELIMU WANAFUNZI WENYE ULEMAVU

WAZAZI NA WALEZI WATAKIWA KUWAPA NAFASI YA KUPATA ELIMU WANAFUNZI WENYE ULEMAVU

Na Shomari Binda-Musoma

WAZAZI na walezi wametakiwa kuwapa nafasi watoto wenye changamoto ya ulemavu mbalimbali kupata elimu kuanzia msingi hadi vyuoni.

Naibu Meya wa manispaa ya Musoma Naima Minga kwa niaba ya Meya Patrick Gumbo amesema kila mtoto anastahiki kupata elimu wakiwemo wenye ulemavu.

Hotuba yake ya maafali ya 20 ya shule ya msingi Mwisenge B amesema serikali ya Rais Dkt,Samia Suluhu Hassan imekuwa ikisisitiza suala la elimu hasa kwa makundi maalumu kwa kuwa nao wanastahili.

Naima amesema watoto wenye ulemavu wakupewa nafasi ya kupata elimu wanayo nafasi ya kufanya vizuri katika maeneo mengine.

Amesema wapo watu wenye ulemavu ambao leo walifanikiwa kupata elimu na leo wanafanya kazi serikalini na taasisi binafsi.

“Niwapongeze sana wahitimu wa darasa la 7 hapa shule ya Mwisenge B ambayo ina historia kubwa hapa nchini”

“Hii ni shule ambayo pia ni shule maalumu kwa wanaoishi na ulemavu mbalimbali hivyo nitoe wito kwa wazazi na walezi kuwapa kuwapa nafasi watoto wenye ulemavu” amesema.

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Mwisenge B Mwita Sigawa amesema namna walivyowaandaa vizuri wanafunzi wakiwemo wenye ulemavu wana uhakika wa kufanya vizuri kwenye mtihani wao.

Katika risala yao wahitimu wa darasa la 7 wa shule hiyo wamewshukuru walimu wao kwa kuwapa elimu bora na wana uhakika wa kufanya vizuri.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!