Na Magrethy Katengu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema bado bara hili limeendelea kukabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo, uhaba wa chakula,viwango vikubwa vya ukosefu wa ajira, umaskinil uliokithiri na ukosefu wa usawa kwenye jamii.

Rais Dkt Samia ameyasema hayo Leo katika Mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika uliobeba Kaulimbiu ya ‘’Kuchochea Ukuaji wa Uchumi Afrika: Kuongeza Uzalishaji wa vijana kipitia mafunzo na ujuzi yani
“Accelerating Africa’s Economic Growth: Boosting Youth Productivity by Improving Learning and Skills” Mijadala ilikuwa ujadili ikihusu mtaji wa rasilimali watu ambapo inaonekana Afrika Ina idadi kubwa ya vijana ni fursa ya pekee katika mageuzi ya uchumi.
“Ni wazi kuwa Bara letu bado linahitaji mageuzi makubwa katika nyanja zote muhimu za uzalishaji na maendeleo. Na haya ndio malengo na madhumuni ya ajenda ya Maendeleo ya Afrika tunayoitaka ya mwaka 2063 ambayo imeweka malengo 7″ mesema Rais Dkt Samia.
“Nataka nijielekeze kuyazungumzia malengo manne, ambayo ni Afrika ambayo mafanikio yake yanajikita kwenye ukuaji jumuishi wa uchumi na maendeleo endelevu, Bara lenye utangamano kisiasa kwa kuzingatia fikra za kimajumuishi na mwelekeo wa kimapinduzi, Afrika inayozingatia misingi ya utawala bora, demokrasia, haki za binadamu na utawala wa sheria na Afrika ambayo maendeleo yake yanatokana na watu kwa kutumia vipaji vyao, hususan wanawake na vijana pamoja na kutoa makuzi bora kwa watoto” amesema Rais
Mbali na masuala ya rasilimali watu hususan kwa vijana, mkutano huo ulizungumzia pia sekta ya elimu, afya, kilimo, fedha na sayansi na teknolojia ambapo zimejadiliwa kama wazalishaji wa rasilimali watu.
“Idadi kubwa ya vijana tuliyonayo ni fursa ya kipekee katika ukuaji wa uchumi katika bara letu kuliko kuwaacha vijana Hawa kwenda kutafuta fursa ulaya na kupata tabu njiani tuwawezeshe Kwani Maisha Bora yapo Afrika” amesema Dkt. Samia
Amesema swala la maendeleo ya rasilimali watu Afrika haliwezi kuja Kwa kubahatisha na Halima mbadala hivyo ni lazima kuweka mipango madhubuti kuhakikisha rasilimali watu Afrika inaendelezwa Kwa maslahi ya bara na maendeleo ya nchi.
Amesema katika kuhakikisha Taifa la Tanzania linalinda na Kutunza rasilimali watu nchi imechukua hatua mbalimbali ikiwemo kutenga Fedha kwenye Afua za lishe na kulinda Afya ya mama na mtoto lakini pia kuanzisha vituo vya watoto.
Ameongeza kuwa uanzishwaji wa mfuko wa kupunguza umaskini TASAF lakini pia mfuko wa kusaidia vijana kiuchumi pamoja na kuwarudisha wanafunzi waliopata mimba shuleni baada ya kujifungua.
Kwa upande wake Makamu wa rais wa Benki ya Dunia Dkt. Victoria Kwakwa amesema nchi za Afrika zinachangamoto kubwa ya elimu Kwani watoto wa Afrika kusini mwa jangwa la sahara asilimia 80 hawajui kusoma Wala kuandika hivyo kupitia mkutano huu iwekwe mikakati madhubuti ya kuwasadia kwani itapunguza umasikini katika bara la Afrila
“Uganda imekua ya kwanza Kwa kuondoa udumavu kwenye maendeleo endelevu na Kenya imeboresha kwa asilimia 50 katika sekta ya elimu” amesema Kwakwa
Aidha Dr. Kwakwa ameipongeza Tanzania Kwa kufanya mageuzi makubwa katika sekta ya elimu kwa kuwarudisha shuleni wanafunzi waliopata mimba shuleni baada ya kujifungua kuondoa ada kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha nne huku wanajiunga na vyuo vikuu wakipatiwa mikopo ili wasiishie njiani.
Sambamba na hayo amesema zàidi ya asilimia 50 ya walimu hawafundishi vizuri hivyo Kuna haja ya kutenga Fedha kwa ajili ya kujiendeleza kimasomo kuboresha miundombinu ya walimu ili kufikia maendeleo na kuboresha sekta ya rasilimali.
