Na Magrethy Katengu
Kamisha wa Jeshi la Polisi Suzan Kaganda amewashauri Wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kusaidia hali ya ulinzi na usalama kuimarika kwani Jeshi haliwezi kufanya kazi peke yao ya kudhibiti wahalifu pasipo wao .
Amayasema hayo Jijini Dar es salaam alipotembelea Vitengo mbalimbali vya Jeshi la Polisi katika banda la sabasaba ambapo amesema katika ushiriki wao kama. Jeshi wamekuwa wakitoa elimu kuhusu kazi za polisi kwani kufanya hivyo ni kusogeza usalama kwa jamii kufahamu haki zao wanapofika kituo cha Polisi
“Shughuli zetu za kiuperesheni hususani Usalama barabarani tumeweza kuwajulisha wananchi jinsi gani Jeshi lao linavyofanya kazi kwa usawa na weledi kwani hivi karibuni Serikali ilitoa tamko juu ya vyombo vya usafirishaji abiria masaa 24 tumejipanga yeyote atakayekiuka Sheria za usalama barabarani tutamchukulia hatua Kali za kisheria” amesema Kamishna Kaganda
Naye Afisa Muuguzi kutoka Kituo cha Afya kilichopo Kilwa road Dr es salaam ASP Asia Ngamange amesema Jeshi la polisi pia wanahuduma ya kuhudumia wagonjwa katika hospitali zao mbalimbali nchini na katika banda lao wamekuwa wakitoa huduma mbalimbali ikiwemo kupima Afya kutoa ushauri nasaha hivyo wananchi wanaalikwa kufika kujua afya zao na ni bure .
Kwa Upande wake Ofisa Mfiziotherapia Inspekta Focus Magenge amesema katika maonyesho hayo banda lao licha ya kutoa elimu ya kuhusu uhalifu lakini pia huduma za afya zilizokuwa iliuokuwa inatolewa kila suku imekuwa ikiigusa jamii ikiwemo huduma ya kupima presha,kisukari,virusi vya ukimwi, na wananchi wamejitokeza kwa wingi.
Mrakibu Msaidizi wa Polisi Msimamizi Dawati la usalama kwanza ASP Manase Dotto amesema kuwa kitengo hiko ni programu iliyoanzishwa na jamii Polisi na Watoto kuwafikia popote walipo. ikiwemo Shuleni, nyumbani na kwenye nyumba za ibada lengo kushirikiana na wadau wenye malezi na watoto kuwapatia elimu namna ya kuwafundisha kujiepusha na uhalifu.









