Na Magrethy Katengu
JESHI la polisi Tanzania katika maonyesho ya biashara sabasaba watoa Elimu ya Masuala mbalimbali kwa wananchi kupitia vitengo vyao ikiwemo Dawati la Usalama wetu kwanza,dawati la watoto na jinsia, polisi jamii, kupambana na dawa za kulevya.
Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es salaam katika banda lao sabasaba Mrakibu Msaidizi wa Polisi Msimamizi Dawati la usalama kwanza ASP Manase Dotto amesema kuwa kitengo hiko ni programu iliyoanzishwa na jamii Polisi na Watoto kuwafikia popote walipo. ikiwemo Shuleni, nyumbani na kwenye nyumba za ibada lengo kushirikiana na wadau wenye malezi na watoto kuwapatia elimu namna ya kuwafundisha kujiepusha na uhalifu.
“Tangu tumeanza programu hii imekuwa na mafanikio makubwa kwa watoto kumwona polisi ni adui. hata wanapokumbana na changamoto zinazosababishwa na. jamii inayowazunguka kushindwa kutoa taarifa ili wasaidiwe lakini sasa tunakwenda huko waliko tunaawafanya marafiki zetu na kuwapatia mbinu za kujikinga na uhalifu na kutoa taarifa za uhalifu na wale waliokuwa watukutu ambao hawaendi shule tumewabadilisha mienendo yao”amesema ASP Manase
Sambamba na hayo amesema baadhi ya watoto wa kike wamekuwa na changamoto miongoni mwa jamii yetu kutendewa vitendo viovu ikiwemo kubakwa na makondakta wa magari,ndugu zao wa karibu hivyo tumewaelimisha na kuwapatia elimu ya kutoa taarifa na wahusika tuliowabaini tumewashughulikia kisheria .
Naye Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Kamisheni ya Makosa ya Jinai Kitengo cha kuzuia na Kupambana na Dawa za kulevya Lucia Munisi amesema wamekuwa katika maonesho hayo kuonesha aina mpya ya wahalifu wanaotumia kuuza au kusambaza dawa za kulevya ikiwemo kutengeneza keki biskuti aina ya chokleti hivyo kila mtu awe makini kuangalia siyo kila zawadi anayopokea ni zawadi vingine ni dawa za kulevya hivyo wawe makini .
“Nawasisitiza Wazazi wawe na utaratibu wa kuwakagua watoto wao mara kwa mara katika mabegi yao ya shule wengine wametumiwa kupeleka mizigo mahali wakijua ni keki kumbe wamebebeshwa dawa za kulevya na wawazuie watoto kupokea zawadi holela wasije wakajikuta wametumia dawa za kulevya na zikawaharibu mienendo yao ” amesema Lucia
Sanjari na hayo amesema matumizi ya dawa za kulevya ni hatari kiafya kwani inasababisha ikiwemo kuugua saratani na koo , kukosa usingizi hivyo bangi, mirungi, kokeini, visitumiwe wala kuguswa kwani vijana walio wengi wameathirika kisaikolojia wengine wamekuwa vichaa kutokana na matumizi ya hayo madawa
Kwa upande wake Mrakibu wa Jeshi Polisi. Kutoka Kamisheni ya Polisi. Jamii Kitengo cha ushirikishwaji Dkt Ezekiel Kiyogo amesema katika siku hizi za Maonyesho. sababa wamewapatia elimu ya kutosha wananchi kutambua kuwa nao wanahusika. katika ulinzi na usalama katika mali zao kwani wao ndiyo wahusika wakuu wanaweza kusaidia upatikanaji wa taarifa za wahalifu hivyo lazima wawe karibu na Jeshi la polisi kushirikiana kudhibiti wahalifu








