Na Magrethy Katengu
Mamlaka ya Usafiri Ardhini LATRA imewataka Madereva wote kwenda Banda la Mainyesho kusajiliwa katika mfumo kabla ya Julai 30 mwaka huu kisha kufanya mitihani na kupewa vyeti kwani baada ya hapo hatoruhusiwa Dereva kufanya kazi hiyo kama hajasajiliwa .
Akizungumza na katika Banda lao ya sabasaba Kaimu Mkuu cha Mahusiano Salum Pazzi ambapo amesema wamefanikiwa kushiriki Maonyesho ya biashara sabasaba na wamewafikishia huduma mbalimbali wanazozitoa ikiwemo ni usajili wa madereva kwani hao wamepewa dhamana kushikilia maisha ya abiria na pia Mali na kusafirisha mizigo mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi
“Kwa mujibu wa Sheria ya Latra ya kifungu namba (3) iliyotungwa mwaka 2019 kupewa jukumu la kuwapitisha madereva wote wanaotumia vyombo vya usafiri vya kibiashara kuwasajili hivyo itakapofika Julai 30 ,2023 muda ulitolewa utakuwa umefikia kikomo wawe ndani ya kanzi data ya Latra ili tufahamu nani na nani wanafanya kazi ya udereva “amesema Pazzi
Hata hivyo amesema watakaosajiliwa watapata nafasi ya kufanya mtihani na baada ya tarehe hiyo ya usajili kufikia kikomo haitoruhusiwa dereva yeyote kufanya kazi hiyo na akibainika hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake hivyo wamerahisishiwa katika Banda la sabasaba wafike na kuna vifaa maalumu na watachukuliwa taarifa zao kwa mfumo wa vidole na wakitaka kufanya mtihani kuna vituo katika mikoa yote kufanya mitihani.
Sambamba na hayo amesema kuwa katika Banda lao wadau wafike waone mfumo(VTS) unaofuatilia mwendokasi wa magari jinsi unavyafanya kazi na mabasi yote yaliyo katika mfumo huo kuna mishale inaonyesha mwekundu ni hali ya kuzidiasha mwendo na kijani unaonyesha hali ni shwari








