Na Shomari Binda-Musoma
MBUNGE wa jimbo la Musoma mjini, Vedaatus Mathayo, kesho anakutana na vijana we jimbo hilo kuzungumzia shughuli za maendeleo ikiwemo miradi ya kiuchumi.
Akizungumzia lengo la kikao hicho mbunge huyo amesema ni kukutana na vijana wote kuweza kuwasikiliza na kujua changamoto zao.
Amesema amekuwa na utaratibu wa kukutana na vijana na kujadiliana na kuwajengea uwezo wa kufanya shughuli za kiuchumi wanazoweza kuzifanya.
Mathayo amesema hivi karibuni amefanya ziara ya kuzunguka Kata zote za jimbo hilo na kuzungumza nao kuhusu miradi ya ufugaji wa kuku na samaki kwa njia ya vizimba.
” Lengo ni kukutana na makundi mbalimbali kama muendelezo wa kujadiliana kwa pamoja na kesho tunaanza kukutana na vijana wetu.
” Vijana wanayo mambo yao wito wangu kesho wafike tuzungumze kwa pamoja masuala mbalimbali yanayowahusu“amesema Mathayo.
Amesema kikao hicho ni cha vijana wote bila kujali itikadi zao hivyo kila mmoja anapaswa kufika na wazo la kila mtu litasikilizwa.
Aidha ofisi ya mbunge huyo imewakumbusha vijana kufikabkwenye kikao hicho kwa kuwa kuna masuala muhimu ya kujadiliana.
Amesema kikao hicho cha kesho kitakachofanyika kwenye ukumbi wa CCM mkoa kuanzia majira ya saa 9 alasiri kitakuwa na mjadala wa pamoja.








