Home Kitaifa MUHONGO APELEKA MAOMBI HALMASHAURI IKAMILISHE MIRADI YA MAENDELEO

MUHONGO APELEKA MAOMBI HALMASHAURI IKAMILISHE MIRADI YA MAENDELEO

Na Shomari Binda-Musoma

MBUNGE wa jimbo la Musoma vijijini,Profesa Sospeter Muhongo, ameiomba halmashauri ya Wilaya ya Musoma ikamilishe miradi mikubwa ya maendeleo iliyopo.

Moja ya miradi hiyo ni ujenzi wa hospital ya Wilaya inayojengwa kwenye Kitongoji cha Kwikonero Kijiji cha Suguti ambapo serikali imetoa fedha nyingi.

Amesema kukamilika kwa hospitai hiyo kutasaidia huduma za afya kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kutembea umbali mrefu.

Amesema mradi mwingine mkubwa ni ujenzi wa makao makuu ya halmashauri inayojengwa hapo hapo Kwikonero ili iweze kukamilika.

Muhongo amesema vipo vituo vya afya vilivyojengwa chini ya kiwango virekebishwe na kukamilishwa ambavyo ni vile vya Mugango na Bugwema.

Amesema halmashauri itekeleze ipasavyo miradi ya maendeleo ya vijiji kwa kutumia mapato yake ya ndani ambayo juhudi za makusanyo zinapaswa kufanyika.

Mbunge huyo amesisitiza halmashauri inapaswa ijiepushe kupata hati chafu ambazo hazikubaliki kwa wananchi na kupata maelezo ya hati hizo.

Aidha ameomba halmashauri itambue michango ya wadau wa maendeleo ikiwemo ya mbunge na michango ya wanavijiji (nguvukazi zao) kwenye miradi ya maendeleo inayotekelezwa vijijini mwetu na kuomba ripoti za matumizi mabaya ya fedha za umma zitolewe haraka.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!