Home Kitaifa WANANCHI WAAGA MWILI WA JENISTA MHAGAMA

WANANCHI WAAGA MWILI WA JENISTA MHAGAMA

Na Asella Denis

Mamia ya wananchi wamejitokeza kushiriki misa ya kumuombea na kuuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Jenista Mhagama. Ibada hiyo imefanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Benedict lililopo Abasia ya Peramiho, Parokia ya Peramiho, Jimbo Kuu la Songea.

Misa hiyo imehudhuriwa na viongozi wa Serikali, wanasiasa, viongozi wa dini pamoja na waumini na wananchi mbalimbali waliofika kutoa heshima zao za mwisho kwa marehemu. Tukio hilo limekuwa sehemu ya taratibu za kumuenzi na kutambua mchango wa Jenista Mhagama katika uongozi na maendeleo ya jamii ya mkoa wa Ruvuma.

Baada ya ibada, mwili wa marehemu umepangwa kupelekwa nyumbani kwake Parangu, Peramiho, Songea, kabla ya kesho, Desemba 16, 2025, kusafirishwa asubuhi kuelekea kijiji cha Ruanda, wilayani Mbinga, mkoani Ruvuma, kwa ajili ya mazishi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!