Home Kitaifa SERIKALI YAUNDA TUME KUCHUNGUZA UVUNJIFU WA AMANI, OKTOBA 29

SERIKALI YAUNDA TUME KUCHUNGUZA UVUNJIFU WA AMANI, OKTOBA 29

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Jumanne Novemba 18, 2025 kwa mamlaka aliyonayo ameunda Tume huru ya kufanya uchunguzi wa matukio ya Uvunjifu wa amani yaliyotokea nchini wakati na baada ya uchaguzi Mkuu wa Jumatano Oktoba 29, 2025.

Katika taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu Mstaafu wa mahakama ya Tanzania ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo.

Wajumbe watakaofanya kazi na Jaji mstaafu Chande ni pamoja na Profesa Ibrahim Hamis Juma, Jaji Mkuu mstaafu wa Mahakama ya Tanzania, Balozi Ombeni Yohana Sefue, Mwanadiplomasia na Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu na Balozi Radhia Msuya, Mwanadiplomasia na Balozi Mstaafu.

Wengine ni Balozi Luteni Generali Paul Meela, Mwanadiplomasia na Balozi mstaafu, Mkuu wa Jeshi la Polisi mstaafu IGP Said Ally Mwema, Balozi David Kapya, Mwanadiplomasia na Balozi mstaafu na Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax, Katibu Mtendaji mstaafu wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC).

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!