Mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi UVCCM taifa Mohamed Kawaida akiwa na Makamu wake Rehema Sumbo Leo kwa mara ya kwanza Wamekutana na vijana wa jijini la Dar es salaamu.

Hii ikiwa ni baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho 27 Novemba 2022.
Vijana wa wilaya zote ndani ya Jiji la Dar es salaam, zimeshiriki katika zoezi la kumpokea mwenyekiti wa UVCCM wakishirikiana na uongozi wa vijana Tanzania bara na kutoa burudani mbalimbali.
Hata hivyo makamu Mwenyekiti wa Uvccm taifa amewasihi vijana kuendelea kuchapa kazi kwa bidii huku akiwaahidi kuwapambania katika nafasi za ajira.
“Wasio elewa hawaelewi lakini sisi waelewa tunaelewa nini umuhimu wa mradi wa mwalimu Julias Nyerere, utaende kuondoka adha ya umeme kwa vijana wanao fanya kazi kwa kutegemea umeme“

Comdred Kawaida amesema kuwa anawashangaa baadhi ya vijana ambao wanasemea vibaya kazi wanayoifanya Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan na kwani miradi hii ndio vijana wanapopata nafsi ya ajira
Pia amewakumbusha vijana wa Uvccm kuvunja makundi kwani uchaguzi ushaisha na Sasa ni wakati wa vijana kufanya kazi wakisaidiana na Viongozi wao kuanzia kata mpaka Taifa.